Monday , 5th Sep , 2016

Msanii wa bongo fleva anayetamba na ngoma yake ‘Mboga Saba’ Mr Blue amesema yuko atamchukulia hatua za kisheria mtu aliyesambaza habari za kuwa anawasiliana na mpenzi wake wa zamani Naj.

Mr Blue

Akiongea ndani ya eNews Rapa huyo amesema yeye binafsi hakuwasiliana na Naj, isipokuwa habari hizo zilipoanza alidhani ni kiki inayotengenezwa na Naj pamoja na mpenzi wake Baraka The Prince, ili kuachia wimbo wao wa pamoja.

“Ile habari ilikuwa ya uongo, mwanzoni mi nilihisi Baraka na mchumba wake Najma watakuwa wameitengeneza kwa ajili ya mambo yao ya kutafuta kiki, kwa sasabu ilisemekana kuna nyimbo yao wanataka kutoa Baraka na Najma, kwa hiyo wanatafuta kiki kutumia ubavu wangu, nikabahatika kukutana na Baraka na kumshika mkono, na kumwambia akubali mbele za watu, akasema hajui hiyo taarifa”, Mr Blue alionge ndani ya eNews.

Pia alisema, "Hatua za kisheria lazima zichukuliwe, mi siwezi kurudia matapishi ambayo nishawahi kuyatapika, eti nikampigie Najma sijui niwe naye, mimi najua mke wa kumuoa najua mwanamke wa kuwa naye ndiyo maana nikamchagua mke wangu, siwezi tena kufikiria eti kumpigia Najma, siwezi kufikiria kugombana na Baraka, kwanza hatulingani, wakati naanza muziki yeye bado yuko shule anasoma, kama ni kweli ni wao japokuwa Baraka amenithibitishia siyo wao, nikijua ni wao lazima nitafute njia ya kuwashikisha adabu”.

Baraka The Prince na Naj