
Kwenye ukurusa wake wa Instagram Paul amepost picha ikimuonesha amesimama na kaka yao Jude Okoye huku wakiwa wamekata sehemu aliyosimama Peter na kuweka picha ya studio, huku akiandika maneno ambayo moja kwa moja yalikuwa yanamlenga ndugu yake Peter, na kuonesha kuwa anamuunga mkono kaka yao Jude.
"This is where I belong and this is where I stand.......you do music in the studio, not on social media, you have family issues, you discuss that in close doors, not on social media ..... Family is family, blood is blood .... If you don't do family business, then who am I to you?
Akimaanisha (hapa ndipo ninapostahili na ndipo ninaposimama, unafanya muziki studio na sio kwenye mitandao ya kijamii, una masuala ya kifamilia, unayajadili ndani ya nyumba, sio kwenye mitandao....familia ni familia, damu ni damu, kama haufanyi biashara za familia, basi mimi ni nani kwako?), alisema Paul kwenye ukurasa wake wa Instagram
Baada ya muda mfupi Peter alichukua picha hiyo na kujibu kile kaka yake alichokiandika na kusema haya....
....."And cutting me off from a picture and replacing me with a studio set says it all my bro. All because you want to sound matured and letting the pple insult and Laff at me. Peter Okoye the social media rant. I wish you well in all you do my bro. God bless our hustle.
Akimaanisha ( Kunikata kwenye picha na kuweka studio badala yangu inamaanisha yote kaka yangu, yote kwa sababu unataka kuonekana umekua, na kuruhusu watu wanitusi na kunicheka, nawatakia kila la kheri kwenye unalofanya kaka yangu, Mungu abariki mihangaiko yetu), aliandika Peter.
Hivi karibuni Peter aliibua gumzo kwenye mtandao wa twitter na kuandika kuhusu wao P square, na kutaka kaka yao Jude anayewaongoza, awaache kwani anawatumia na kufaidika yeye, huku akisisitiza kuwa hataki kufanya biashara za familia.