
Pancho Latino
Latino amefunguka hayo na kusema kuwa amekuwa akirekodi na kupatana na wasanii kwamba baada ya show alipwe kiasi fulani lakini matokeo yake mambo yanakuwa tofauti na hata baadaye kinachofuata huwa ni 'Producer' kunyonywa na msanii kuwa na maendeleo makubwa.
"Niliamua kutofanya kazi na wasanii tofauti tofauti kwa sababu mwisho wa siku niligungua natumika bila kujijua kiasi kwamba mtu anakuja studio mnarekodi vizuri mnapatana nyimbo ikitoka baada ya show atakuletea kiasi kadhaa lakini hafanyi hivyo, anakuja mara ya pili anakuongopea the same lies au tofauti, unakuja kugundua producer hauna maendeleo msanii ana maendeleo” - Pancho Latino
Hata hivyo Latino ameongeza kuwa, wasanii wengi katika lebo yake kuondoka nalo ni jambo ambalo limemfanya aamue kutulia kimya ili kujipanga kufanya mapinduzi katika sanaa.
Latino amewahi kutamba baada ya kutengeneza ngoma nyingi kali za wasanii tofauti tofauti kama Joh Makini, Mabeste Vanessa Mdee na wengine wengi kwenye studio za B'Hits.