
Rais Kikwete akiaga mwili wa Marehemu Kapteni Komba leo
Akiongea kabla ya kuuaga mwili wa Marehemu Kaptein John Komba, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda amesema bunge la Tanzania litamkumbuka marehemu kwa uhodari wa vipaji alivyokuwa navyo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na familia inaonyesha kuwa mwili wa marehemu Kapteni Komba ambaye alifariki dunia siku ya jumamosi, utasafirishwa leo kuelekea kijijini kwao Lituhi wilayani Songea Mkoani Ruvuma kwa ajili ya mazishi ambayo yamepangwa kufanyika kesho.