Tuesday , 18th Mar , 2014

Kufuatia sakata la msanii Nazizi kuripotiwa na vyombo mbalimbali kuachana na mume wake na kuanzisha mahusiano mapya na mtayarishaji muziki kutoka Tanzania Kheri Sappy, wawili hawa wamekanusha na kusema ni uzushi mtupu.

Ushahidi ulioshikiliwa kuupatia nguvu uvumi huu, ni picha nyingi za pamoja za Nazizi pamoja na Sappy, picha ambazo Nazizi amesema ni za ushikaji tu ambapo ameongeza kuwa, yeye ana washkaji kibao ambao ni wanaume na huwa haoni tabu kupiga nao picha pale wanapojisikia.

Tumepata pia nafasi ya kuongea na Sappy mwenyewe kuhusiana na swala hili, na haya yakawa ndio maelezo yake kwa watu ambao walianza kuamini tayari kuwa anatoka na Nazizi;