
Msanii kutoka kampuni ya Weusi Nikki wa Pili
Nikki amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya yeye kuchaguliwa kuwa miongoni mwa wasanii wa kusimamia mfuko wa wasanii wa bongo fleva ambao utawasaidia wasanii watakao kuwa wanahitaji fedha kutoka katika mfuko huo.
"Wasanii ambao wanapuuzia kuja katika vikao nawaambia haki zao zitachelewa kuja, mpaka pale mtakapoamua kukaa mstari wa mbele haki ndipo zitakuja lakini mkiendelea kukaa hivyo mtatoa nafasi kwa watu wengine kutengeneza sheria ambazo zitakuja kuwaathiri", alisema Nikki wa Pili.
Mtazame hapa anavyofunguka mengine zaidi.