Thursday , 13th Oct , 2016

Msanii Darasa ambaye amerudi kwa nguvu zote kwenye game ya hip hop ya bongo, amesema suala la wasanii wa sasa kusema wanafanya muziki wa biashara na siyo ule muziki unaoishi, wanakuwa wanakosea.

Darasa

Darasa ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV, na kusema msanii mzuri ni yule anayefanya muziki mzuri na kuacha ujiuze wenyewe kwenye biashara.

“Ni tatizo kubwa sana kwa msanii ambaye anasikika anasema hivyo mbele ya mashabiki au mbele ya mdau, kuna biashara siyo lazima umwambie mtu mi nafanya biashara hata kama unataka kufanya biashara, kwanza lazima ujali feelings, tunatengeneza muziki kwa ajili ya watu na naamini maisha yetu yanakuja kutegemea hivyo, wale watu watacare baada ya wewe kuwatengenezea production nzuri”, alisema Darasa.

Darasa aliendelea kusema kwa upande wake yeye anafanya muziki mzuri na ndiyo maana ameweza kukaa kwenye game kwa muda mrefu na kurudi kwa heshima kubwa.

“Mi nafanya muziki mzuri ndiyo maana sijawahi kusikika nikimwambia mtu nafanya biashara, nime'change' game yangu natengeneza muziki mzuri ambao unawafaa watu wangu, najua wao wata'care, nitaifanya sanaa yangu kuwa sehemu nzuri ya kuishi kwa mashabiki mpaka mimi mwenyewe”, alisema Darasa.