Thursday , 16th Jun , 2016

Mwanamuziki na dansa maarufu nchini Super Nyamwela, ametangaza rasmi kuanzisha kikundi chake cha ngoma za asili ambcho pamoja na ngoma za asili, kitakuwa na watu ambao watakuwa wanachezea vitu mbalimbali kama vile nyoka na moto.

Super Nyamwela

Dansa machachari ameiambia Enews kuwa hana tatizo kabisa na bendi yake ya Twaga Pepeta na kukanusha maneno yanayozagaa mitandaoni kwamba hakuwepo katika show yao ya Mwanza.

Super Nyamela amesema kwamba anatarajia kuanzisha kikundi chake cha ngoma za jadi ambacho hakitaathiri kazi yake ya Twanga na kusema atakuwa akijishughulisha na kazi za kikundi chake muda wake wa ziada.

Amemalizia kwa kusema kwamba watakuwa wanapiga ngoma hizo popote watakapo alikwa.

Kuhusu kukosekana katika show ya Mwanza, Nymwela amesema kuwa yeye na wenzake walikuwa Australia kwa ajili ya kuanza kazi hiyo mpya ya kikundi cha ngoma.