Thursday , 8th Feb , 2018

Mchekeshaji wa filamu na muigizaji wa bongo 'movie' nchini Idris Sultan amefunguka na kudai anawachukia wasanii jinsia ya kike wanaokaa utupu katika video zao kwa lengo la kujitafutia umaarufu wa haraka katika jamii jambo ambalo sio zuri.

Idris amebainisha hayo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri wakati alipokuwa anajibu swali la miongoni mwa mashabiki zake waliotaka kufahamu ni msanii gani hampendi kwa hapa bongo.

"Sio kwamba simpendi, ipo hivi naweza nikawa sikubaliana na fikra zao kwa mida kadhaa lakini naona wengi wao wanabadilika. Nilikuwa sikubaliani na fikra za wasanii sana sana wasichana ambao wanaamua kuchukua umaarufu kwa kukaa tupu tupu basi. Kwa sababu wanapitia njia ambayo wanajifanya 'model', 'video vixen' na mwisho wanashafulia watu ambao wapo katika hiyo category", amesema Idris.

Pamoja na hayo, Idriss ameendelea kwa kusema "kwa hiyo siko 'neutral' kusema hakuna ambaye nina mchukia kusema kweli wapo katika 'level' hiyo lakini naona kama wanakua kwa mfano Gigy Money anafanya vizuri sasa hivi amekua na kazi zake nazipenda kiukweli".

Kwa upande mwingine, Idriss amesema angalau kidogo wasanii ambao walikuwa wanamkera katika ufanyaji kazi zao kwa sasa wanaanza kubadilika.

 

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.