Tuesday , 22nd Aug , 2017

Msanii Roma ambaye hivi sasa amekuwa gumzo kila kona, amefunguka mambo kibao usiyoyajua kuhusu yeye, huku akimjibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuhusu kauli yake ya kuwataka wasanii kuacha kuimba siasa.

Msanii Roma Mkatoliki akiwa studio za East Africa Radio

Akizungumza Exclusive na mwandishi wa East Africa Television, Roma amesema hawezi kuacha kuimba siasa kwani siasa ni maisha ya kila siku, huku akiitaka serikali kuwapa uhuru wasanii kufanya kile wakipendacho kwenye sanaa yao.

Mtazame hapa chini akimpa makavu Mwakyembe.