Thursday , 27th Oct , 2016

Mkongwe wa muziki wa wa bongo Mzee Zahir Zorro amewataka wasanii wa muziki Tanzania kupunguza kuimba matusi katika nyimbo zao wakidhani wanatumia tafsida katika utunzi wa nyimbo zao.

Zahir Zorro

 

Akipiga story ndani ya eNewz Zorro amesema kuna kiswahili cha Dar es salaam ambacho kwa watu ambao wamezaliwa huku tunakuwa tunakijua vizuri hivyo hata ukiimba wimbo kwa kutumia maneno hayo tunakuwa tunaelewa na hayajengi jamii.

Pia Mzee Zahir Zorro alisisitiza kwamba endapo msanii anataka yeye amtungie nyimbo atamtungia lakini siyo kwa kutunga matusi au kutukana katika nyimbo hivyo anawasihi wasanii kuenzi utunzi wa zamani.