Kutokana na hali hii watu maarufu akiwepo Madonna, Kim Kardashian, Puff Daddy na wengine wengi, wameungana na kampeni ya "#BringBackOurGirls" yenye lengo la kutoa msukumo kwa hatua za ziada kuchukuliwa ili kuokolewa kwa wanafunzi hawa.
Wasanii wa Afrika pia akiwepo Victoria Kimani wa Kenya, Banky W, 2 Face, D Banj na wengineo pia, wamekuwa sehemu ya mpango huu kuhamasisha serikali ya Nigeria kutumia kila njia inayowezekana kuokoa wasichana hawa na pia kuondosha uhalifu wa namna hii na wahusika wake.
eNewz inaungana na wadau na wanaharakati wengine wote ndani na nje ya Afrika katika kampeni hii na kulaani pia kitendo hiki cha kinyama ambacho wamefanyiwa wasichana hawa wadogo wa shule.