Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Mnyoo wa 15cm watolewa jichoni mwa binadamu

Thursday , 11th Oct , 2018

Jopo la madaktari nchini India wamefanikiwa kuondoa mnyoo mwenye urefu wa Sentimita 15 kutoka kwenye jicho la mwanaume mmoja nchini humo kufuatia oparesheni iliyofanyika.

Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 60 ambaye jina lake halijajulikana, alikuwa akisumbuliwa na tatizo la macho kuuma  kwa muda mrefu ndipo alipoamua kwenda kuwaona madaktari hao.

Oparesheni hiyo imefanyika katika jimbo la Karnataka linalopatikana kusini magharibi mwa nchi hiyo, ambapo katika uchunguzi zaidi wa madaktari uligundua kuwa mgonjwa huyo aliathiriwa na minyoo hadi katika damu yake.

Mmoja wa madaktari waliohusika katika oparesheni hiyo, Dr.Srikanth Shetty amesema,

'" Changamoto ilikuwa ni kumtoa mnyoo huyo mzima, kuepuka kufia katika jicho la mgonjwa huyo, jambo ambalo lingeleta matatizo makubwa zaidi ".

" Na ilikuwa ni ngumu kumbana mnyoo huyo kwasababu alikuwa akitembea tembea katika jicho la mgomjwa. Pia tumegundua kuwa alikuwa na minyoo hadi kwenye damu na tumempatia matibabu yake", ameongeza daktari huyo.

Kwa makadirio, takribani watu millioni 120 katika nchi za Afrika ya kati, kusini na katikati ya bara la Amerika  pamoja na bara la Asia wanaugua magonjwa ya minyoo lakini ni mara chache hutokea minyoo hiyo kuvamia katika macho.

Katika tukio lingine nchini Malaysia, raia mmoja alijikuta katika dalili hizo za macho baada ya kuogelea katika mto wiki kadhaa zilizopita.

HABARI ZAIDI

Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari

Picha ya Diddy na Cassie enzi za mahusiano yake

Diddy aomba msamaha kumshambulia EX wake Cassie

Rais wa Iran Ebrahim Raisi

Rais wa Iran afariki kwa ajali ya Helikopta

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu