Tuesday , 4th Dec , 2018

Rais wa shirikisho la soka nchini (TFF), Wallace Karia amesema kocha wa timu ya taifa ya Tanzanzia Taifa Stars Emmanuel Amunike hastahili lawama kwa kupoteza dhidi ya Lesotho kisa kikosi alichopanga wakati wachezaji wote ni Watanzania.

Wallace Karia

Karia amesema amekuwa akisikia lawama nyingi zikitupwa kwa mwalimu Amunike kutokana na kikosi kilichoanza dhidi ya Lesotho lakini ukweli ni kwamba sio kila mtu anaweza kuwa mwalimu.

Kila mtu anaongea kivyake lakini ukichunguza hata hao wachezaji wanaolalamikiwa hata kwenye timu zao hizo haziwaamini zimekwenda kuchuku straika wa nje ndio wanacheza sasa ikija timu ya taifa wanalalamika'', amesema.

Kuhusu nafasi ya kufuzu Karia anasema uhakika upo kwani tangu uongozi wake uingie madarakani hakuna mechi Taifa Stars imepoteza kwenye uwanja wa taifa hivyo mechi dhidi ya Uganda itashinda na kufuzu.

Kwa upande mwingine Karia amewataka mashabiki kuungana na kuwa kitu kimoja kama timu ilipopoteza mechi dhidi ya Cape Verde na baadaye ikaja kushinda hapa nyumbani.