
Mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza
Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema, kadi kwa ajili ya wachezaji wa Ligi Daraja la Kwanza zilishakamilika na wamewasiliana na viongozi lakini cha kushangaza mpaka muda huu viongozi hao hawajajitokeza kwa ajili ya kuchukua leseni za wachezaji hao na badala yake wameendelea kutumia leseni za muda walizopewa wakati ligi inaanza.
Alfred amesema, leseni hizo zina wiki ya pili sasa tangu zitolewe na bado baadhi ya timu zimeendelea kutumia leseni ambazo haziruhusiwi kwa sasa, hivyo katika mchezo unaofuata wa mzunguko wa tano hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuingia uwanjani kwani bado wana muda wa kufuatilia kadi hizo.