
Kocha Msaidizi wa Azam FC Dennis Kitambi, amesema wanaamini lolote linaweza kutokea katika soka lakini inawabidi kujitahidi kukusanya pointi tatu katika kila mchezo katika mechi zilizobakia ili kuweza kushikilia nafasi ya pili.
Kitambi amesema, katika mchezo wa jana dhidi ya timu ya Simba ambao walitoka sare ya bila kufungana kikosi chake kilicheza kwa uchovu kutokana na kuwa na mechi mfululizo lakini katika kipindi cha pili cha mchezo hawakutaka kuamini kuwa uchovu unachangia kushindwa kufanya vizuri.
Kitambi amesema, kipindi cha pili wachezaji waliweza kupambana na walipata nafasi lakini walishindwa kuzitumia hivyo kupelekea sare ya bila kufungana.
Kwa sasa Yanga wanaongoza ligi kwa wastani wa pointi 65 kuelekea mechi nne za mwisho ikifuatiwa na Azam FC ambayo imefikisha pointi 59 wakati Simba sasa inakuwa na pointi 58 baada ya timu zote kucheza mechi 26.