
Azam FC walipokuwa kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi
Katika mchezo wa leo, Azam imejipatia mabao yake kupitia kwa Shaaban Idd aliyefunga mabao mawili dakika ya 13 na 44, huku bao la tatu likifungwa na Ramadhan Singano 'Messi' mwanzoni kwa kipindi cha pili huku bao la Ndanda likifungwa na William Lucian dakika ya 14
Timu hizo sasa zinasubiri mshindi kati ya Yanga na Prisons mchezo utakaopigwa April 22, mwaka huu, ili kujua ni nani atakutana na nani katika hatua ya nusu fainali.