Tuesday , 21st Jul , 2015

Azam FC imejihakikishia kufuzu katika hatua ya robo fainali katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kombe la Kagame baada ya kuifunga Malakia ya Sudan bao 2-0 Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Azam ilianza kupata bao lake la kwanza katika dakika ya 26 kupitia kwa mchezaji wake John Bocco huku bao la pili likipatikana ndani ya kipindi cha pili katika dakika ya 51 kupitia Kipre Tchetche akipokea pasi kutoka kwa Shomari kapombe.

Katika mchezo mwingine uliopigwa katika dimba la Taifa kuanzia majira ya saa 8 mchana, timu za Al Ahly Shandy imetoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 na timu ya LLB AFC.

Katika uwanja wa Karume timu ya APR ya Rwanda imecheza na Heegan FC ya Somalia ambapo matokeo ni

Mechi za kesho ni Khartoum ya Sudan dhidi ya KMKM ya Zanzibar katika uwanja wa Taifa kuanzia saa 8:00 mchana, KCCA ya Uganda itakutana na Adama City katika dimba la Karume saa 10:00 na Yanga itacheza na Telecom ya Djibout.