Friday , 22nd Jan , 2016

Timu ya taifa ya DR Congo imeungana na wenyeji Rwanda kwenye robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wachezao ligi za ndani kufuatia ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Angola.

Michuano ya CHAN 2016 yazidi kufana nchini Rwanda

Katika mchezo huo wa kundi B uliopigwa huko Stade Huye nchini Rwanda Congo walifunga mabao yao kupitia nyota wake Nelson Munganga, Eli Meshack, Bolingi Mpangi Jonathan na Mervielle Bokadi na Angola kufunga bao zao 2 kupitia Adriano Belmire Duarte.

Congo Dr ambao ndiyo timu iliyotwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast wanafuzu wakiwa na mechi moja mkononi baada ya kushinda mechi yao ya kwanza dhidi ya Ethiopia kwa mabao 3-0 kwenye mechi nyingine ya Kundi B timu za taifa za Cameroon na Ethiopia zilitoka sare tasa yaani 0-0.

Michuano hiyo itaendelea leo kwa mechi mbili za Kundi C huko Stade Régional de Nyamirambo ambapo Tunisia itaivaa Nigeria huku Niger ikiumana na Guinea.