
Mchezo huo, wa kwanza wa kihistoria kuwahi kupigwa nje ya Uingereza, bado haujapangiwa uwanja utakaofanyika, lakini upo kwenye ratiba ya michezo ya mashindano ya International Champions Cup.
Mahasimu hao, walikosa kuchuana nje ya Uingereza mwaka uliopita, kwa mchezo wa kirafiki wa maandalizi ya msimu huu huko Beijing China kutokana na mvua kubwa iliyonyesha.
Manchester City pia itakipiga na vigogo wengine wa ligi ya Uingereza, Tottenham Hotspurs, Mjini Nashville Julai 29, kabla ya kukutana na Real Madrid Jijini Los Angeles Julai 26 .