Tuesday , 26th Jan , 2016

Michuano ya kombe la Shirikisho FA Cup inaendelea hii leo kwa michezo minne kupigwa katika mikoa minne tofauti hapa nchini.

Mtibwa Sugar watawakaribisha Abajalo FC uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Lipuli watacheza dhidi ya JKT Ruvu uwanja wa Wambi Mafinga, Africa Sports wakiwa ugenini dhidi ya Coastal Union Mkwakwani jijini Tanga huku Geita Gold wakiwa wenyeji wa Mgambo Shooting katika uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.

Mtibwa Sugar wanashuka dimbani lakini huenda wakamkosa mshambuliaji wao Shiza Kichuya katika mchezo wa mzunguko wa tatu Kombe la Shirikisho FA utakaochezwa leo Uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Katika taarifa yake Kichuya amesema, anatarajia kuukosa mchezo huo kutokana na kuumia goti katika mchezo wa Ligi kuu dhidi ya Simba SC uliochezwa hivi karibuni Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kichuya amesema, ameanza kufanya mazoezi mepesi jana asubuhi hivyo inakuwa vigumu kucheza mchezo huo kwani kwa sasa hawezi kukimbia na kupiga mashuti kwa kuwa hali yake bado na anaendelea na matibabu.

Kichuya amesema, anatarajia taaanza mazoezi magumu akiwa na kikosi kizima cha Mtibwa Sugar kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.