
Luis Suarez (kushoto) na Phillipe Coutinho (kulia)
Coutinho alihamia kwa vigogo hao wa Catalonia kwa ada ya £ 142m, baada ya kumsajili Luis Suarez kwa ada ya £ 73m kutoka klabu hiyo siku chache baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia mwaka 2014.
Kufuatia hatua hiyo ya kupokonywa wachezaji wake tegemeo na klabu moja, Liverpool kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Michezo, Michael Edward ilikubaliana na Barcelona kuwa katika usajili wowote ambao vigogo hao wa Hispania wataufanya mpaka 2020, watalazimika kulipa Pauni 89 milioni kama nyongeza.
Coutinho ilisainiwa na Barça kama mbadala wa muda mrefu baada ya kuondoka nyota wa Kibrazil, Neymar. Mchezaji huyo wa zamani wa Santos alijiunga na vigogo wa Ufaransa, PSG kwa rekodi ya dunia ya Euro 222m baada ya kipengele chake cha kuuzwa kulipwa na klabu hiyo.
Pamoja na Coutinho, winga wa Ufaransa, Ousmane Dembélé pia alijiunga na Barcelona, akiwa ni mmoja ya wachezaji waliokuja kujaza pengo ambalo liliachwa na Neymar.
Hata hivyo, mshindi huyo wa Kombe la Dunia amejitahidi kukabiliana na maisha katika ya klabu hiyo, huku tayari akihusishwa na kuondoka katika klabu hiyo, mwaka mmoja tu baada ya kusajiliwa kwa € 115m kutoka Borussia Dortmund.
Liverpool na Arsenal pia zinahusishwa kuifukuzia saini ya kinda huyo mwenye umri wa miaka 21 siku za usoni, zikiwa na lengo la kuimarisha vikosi vyao hasa baada ya kuoneka kuanza vizuri katika EPL msimu huu.