Tuesday , 4th Apr , 2017

Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara wa mwezi Machi kwa msimu wa 2016/2017.

Wachezaji wa Kagera Sugar

Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.

Katika mwezi huo ilichezwa raundi moja tu na Mbaraka ambaye alicheza kwa dakika zote 90 aliisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu zilizoifanya timu yake kubaki katika nafasi ya nne (4) katika msimamo wa ligi kwa mwezi huo.

Katika mchezo huo mmoja, Mshambuliaji huyo alifunga goli moja, na alionyesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la kadi.

Mbaraka Yusuph alipoitumikia Taifa Stars kwa mara ya kwanza

Mbaraka Yusuph ndiye mfungaji wa bao la ushindi katika mchezo wa Taifa Stars dhidi ya Burundi katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambapo Taifa Stars ilishinda mabao 2-1.

Kwa kushinda tuzo hiyo, Mbaraka atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo.

Huyu ni mchezaji wa pili kutoka Kagera Sugar kwa msimu huu kupata tuzo hiyo, ikikumbukwa kuwa golikipa Juma Kaseja tayari amekwishapata tuzo hiyo