
Shiza Kichuya akishangilia bao katika mechi dhidi ya Azam FC
Kichuya ambaye ni mshambulaji aliwashinda wachezaji Adam Kingwande wa Stand United na Omari Mponda wa Ndanda FC.
Mchezaji huyo aliisadia timu yake kwa mwezi huo kupata pointi zote 12 katika mechi nne ilizocheza, matokeo ambayo yameifanya Simba iendelee kuongoza ligi hiyo inayoshirikisha timu 16.
Pia alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ilizocheza timu yake.
Kwa kushinda tuzo hiyo ya mwezi, Kichuya atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo, kampuni ya Vodacom Tanzania.