Agizo hilo limetolewa na maarufu kama 'Try again' wakati alipokuwa anazungumzia jinsi walivyoguswa na taarifa za msiba wa nyota wao zamani kama viongozi wa klabu hiyo.
"Marehemu Mambeta ni hazina ambayo Mungu ametupatia lakini sasa Mwenyezi Mungu mwenyewe amepitisha rehema yake kwa hivyo sisi kama Klabu ya Simba kwa masikitiko makubwa tunawaomba wanachama wetu na wapenzi wa wekundu msimbazi tumuenzi mzee huyu", amesema Salim.
Pamoja na hayo, Salim ameendelea kwa kusema "wachezaji wetu wafanye vizuri katika mechi zinazokuja ili kumuenzi shujaa wetu huyu kwani ni moja ya wazee wachache waliokuwa wamebaki katika tasnii hii kwa wazee ambao walifanya vizuri na kuitendea mema klabu".

Kaimu Rais wa wekundu wa Msimbazi Bw. Salim Abdallah
Nyota huyo wa zamani wa Simba, Mzee Arthur Mambeta anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumamosi (Machi 3, 2018) katika makaburi ya maeneo ya Buguruni Jijini Dar es Salaam.





