
Kocha wa Azam (kulia)
Akizungumza jijini Dar es salaam mara baada ya kuwatambulisha wachezaji wapya, Kocha Zeben amesema anatambua malengo yaliyopo ndani ya timu na kwa sasa ameshalisoma soka la Tanzania hivyo anaamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mashindano yote.yaliyombele yao.
Zeben amesema, anaamini kikosi chake kitafanya vizuri zaidi ya Mzunguko wa Kwanza na hata wachezaji wapya waliosajiliwa watafanya kazi katika nafasi zao ili kuhakikisha timu inakaa katika nafasi nzuri zaidi.
Azam FC inayofungua pazia la Mzunguko wa Lala Salama wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara Jumapili dhidi ya African Lyon katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam imewatambulisha wachezaji wake wapya hii leo ambapo wakimataifa ni wanne ambao ni Yakubu Mohamed, Steven Kingue, Samuel Afful, Yahya Mohamed, Enock Agey huku wakimrudisha Joseph Maundi aliyekuwa akiitumikia klabu ya Mbeya City.