
Kushoto ni Arsene Wenger na kulia ni wachezaji wa Liverpool.
Takwimu za Liverpool msimu huu baada ya mechi 19 zinaonekana kuwa juu ya zile za Arsenal msimu wa 2003/04 ambao ilimaliza bila kufungwa.
Mpaka sasa Liverpool ina alama 51 katika nafasi ya 1 wakati Arsenal ilikuwa na alama 45 katika nafasi ya 2.
Katika michezo 19 Arsenal ilikuwa imeshinda mechi 13 pekee wakati Liverpool mpaka sasa imeshinda mechi 16.
Liverpool imefunga mabao 43 na kufungwa 7 pekee kwenye mechi hizo 19, wakati Arsenal kwa kipindi hicho ilifunga mabao 35 na kufungwa 12.
Katika michezo yake 19 msimu huu Liverpool haijaruhusu wavu wake kuguswa kwenye mechi 12, wakati Arsenal ilifanikiwa kumaliza mechi 8 bila mlinda mlango wake kuruhusu bao.
Liverpool inawakaribisha Arsenal wanaoshika nafasi ya 5 msimu huu katika mchezo ambao utaanza saa 2:30 usiku.