Katibu mkuu wa DAREVA Yusuph Mkalambati amesema, viongozi wengi walio ndani ya timu hawajui taratibu na sheria za mchezo huo hivyo kozi hiyo itawasaidia kuweza kukumbuka kitu gani anatakiwa kufanya wakati wa mashindano mbalimbali ya mkoa wa Dar es salaam.
Mkalambati amesema, kozi hiyo pia itaweza klusaidia kuepusha migogoro kati ya viongozi na wachezaji ambayo hutokea pale ambapo mchezaji atajua sheria na kiongozi anakuwa bado hajaelewa vizuri kuhusu sheria za mchezo huo.
Mkalambati amesema, baada ya kumaliza programu hiyo kwa viongozi Februari 21 mwaka huu wanatarajia kuwa na mashindano ya mpira wa wavu ya ufukweni ya mkoa wa Dar es salaam kwa upande wa wanawake mara baada ya kumaliza kwa upande wa wanaume.






