Tuesday , 25th Nov , 2014

Bondia anayeshikilia Ubingwa wa UBO International Continental Africa,Thomas Mashali ametamba kufanya vizuri katika mapambano yake ya mwakani ili kuweza kukuza zaidi kiwango chake katika mchezo huo wa Ngumi.

Bondia Thomas Mashali

Akizungumza na East Africa Radio,Mashali amesema pambano lake la kufungua mwaka anatarajia kupambana na Abdallah Pazzi ambapo anaamini atafanya vizuri japo bondia huyo ameweza kufanya vizuri katika mapambnano yake.

Mashali amesema baada ya pambano hilo anatarajia kupambana mapambano mengine mengi kutoka kwa mabondia wazoefu na wenye uwezo mkubwa ili kuweza kutambua kiwango chake katika kazi yake.