
Kwa ushindi huo, Mbeya City inapanda kileleni mwa Ligi Kuu kwa kufikisha pointi saba baada ya kucheza mechi tatu zote ugenini Kanda ya Ziwa, ikishinda mbili.
Mara baada ya mchezo huo kocha wa City Kinnah Phiri, pamoja na mengine mengi lakini pia aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza vizuri kwa kufuata Maelekezo na hatimaye kuibuka na ushindi huo mnono.
“Vijana wangu wamecheza vizuri, wamefanya kazi kwenye kila tulichokuwa tunakifanyia mazoezi, tulijua Mbao wangekuja na mchezo wa kasi kwa sababu walihitaji sana kushinda hasa baada ya kupoteza mchezo wao uliopita, tunamshukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata pointi saba kwenye michezo yetu mitatu na sasa tunarudi nyumbani kujiandaa na mchzo mwingine”, alisema.