Saturday , 3rd Jun , 2017

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amesema katika mkutano mkuu ujao wa shirikisho hilo watajadili na ikiwezekana kupitisha sheria ya kuamua bingwa kwa kutumia mfumo wa ‘Head to Head’ kama timu mbili za juu zitakuwa zimelingana

Mfumo huo utatumika endapo timu zitalingana kila kitu na lazima bingwa apatikane hivyo watautumia mfumo huo ukiwa na maana wataangalia matokeo ya timu hizo mbili walivyokutana kwenye michezo yao.

“Tumepata funzo kwenye michuano Afrika kwa vijana iliyomalizika hivi karibuni kule Gabon, kama mtakumbuka timu yetu iliondolewa kwa sheria hii baada ya kufungwa na Niger na kujikuta wakiwa na matokeo yaliyofanana…, na sisi tutaingiza mfumo huu kwenye ligi yetu, tutalijadili kwenye mkutano wa TFF,” alisema Malinzi.