
Vikosi vya Simba na Yanga
Wambura amesema wamefanya hivyo ili kupisha michuano hiyo ambayo itaanza April 14 hadi 28 mwaka huu na kufanyika katika viwanja vya Taifa, Uhuru na Azam Complex.
Kwa kawaida timu nyingi za Dar es salaam ukitoa JKT Tanzania ambayo hutumia uwanja wa Meja Jenerali Isamunhyo uliopo Mbweni Dar es salaam, vingine vyote hutumia viwanja hivyo vitatu.
Vilabu vitakavyoathirika ni KMC ambao hutumia uwanja wa Uhuru na Azam Complex, Simba SC na Yanga ambao hutumia uwanja wa Taifa na Uhuru pamoja na Azam FC ambao hutumia uwanja wao wa Azam Complex.
Wambura amesema wakati wa michuano hiyo, Simba itaendelea na ratiba ya kukamilisha michezo yake ya viporo ambayo itakuwa ikicheza viwanja vya ugenini kwa maana nje ya Dar es salaam.
Michuano hii inakuwa funzo kwa vilabu vikubwa vya Simba na Yanga ambavyo kama navyo vingekuwa na viwanja angalau kama ule wa Azam FC basi michuano hii isingeathiri ratiba ya ligi kuu na pengine mechi zao zingeendelea katika viwanja vyao.