Wednesday , 12th Nov , 2014

Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es salam imemuongezea mkataba wa miaka miwili Kiungo wa klabu hiyo Jonas Mkude baada ya kusikika mchezaji huyo ananyemelewa na Klabu ya Yanga na Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam

Mchezaji wa Simba,Jonas Mkude

Klabu ya Soka ya Simba ya jijini Dar es salam imemuongezea mkataba wa miaka miwili Kiungo wa klabu hiyo Jonas Mkude baada ya kusikika mchezaji huyo ananyemelewa na Klabu ya Dar es salam Young Africans maarufu Yanga na Mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania bara Azam FC.

Akiongea jijini leo jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zakaria Hans Pope wakati akitangaza kumuongezea mkataba mchezaji huyo amesema wamefikia uamuzi wa kumuongeza mkataba mkude baada ya kufikia makubaliano aliyoyahitaji licha ya mkataba wa awali wa miaka mitatu kuwa bado hujamalizika.

Kwa Upande Mwingine kuelekea kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili Hans Pope ametangaza kumuwania mchezaji kiungo wa Yanga, Saimon Msuva ili kumsajili kujiunga na kikosi cha klabu ya Simba ili kuimarisha safu ya Ushambuliaji.