Hayo yamethibitishwa na taarifa rasmi zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo jioni ya jana (Aprili 03, 2018) kupitia ukurasa wao maalum wa timu.
Aidha, Job amesema amefurahi kupewa mkataba huo katika timu hiyo na kuahidi kujituma vizuri katika kusaidia timu yake ili iweze kupata matokeo mazuri pindi wanapokuwa dimbani.
Job alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kilichoshiriki fainali za Afrika (AFCON U17) nchini Gabon Mei mwaka 2017 na kwa sasa amepandishwa kwenye kikosi cha U-20, Ngorongoro kinachoshiriki mechi za kufuzu AFCON U-20 mwakani nchini Niger.
Kwa upande mwingine, timu ya Mtibwa Sugar imefuzu kucheza nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho katika siku za hivi karibuni baada ya kuichapa Azam FC kwa mikwaju ya matatu 8-9.







.jpg?itok=0CrdpE0P)