Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi
Licha ya kuwa na na majeruhi wannne kocha msaidizi wa klabu hiyo Juma Mwambusi amesema wamejipanga vyema na wamewaandaa vyema wachezaji wao kushinda mchezo huo wa ugenini ili kupunguza gap yao na Simba.
"Kikosi kinasumbuliwa na Majeruhi lakini waliopo watafanya kazi na tumewaandaa vyema kushinda mchezo huo ugenini". Alisema kocha msaidizi wa klabu hiyo Juma Mwambusi
Katika mchezo wa kesho dhidi ya Majimaji Yanga itawakosa wachezaji wake watano kutokana na kuwa majeruhi mbalimbali akiwemo Donald Dombo Ngoma, Malimi Busungu, Obrey Chirwa, Justin Zullu na Emanuel Martin.
Yanga wanashika nafasi ya pili katika ligi kwa pointi 40 huku Simba wakiwa kileleni kwa pointi 44.