
Mohamed Hussein wa Simba akikabana na mchezaji wa Mbabane Swallows
Tony ameyasema hayo leo baada ya mchezo wa klabu bingwa Afrika hatua ya awali ambapo timu yake imepoteza mbele ya wenyeji Simba mabao 4-1.
''Ni kweli tumepoteza kwa mabao mengi lakini hatujazidiwa sana, tumepotea tu kimchezo nafikiri cha muhimu tuna nafasi ya kubadili matokeo katika mchezo wa marudiano kama wao walivyotumia uwanja wa nyumbani'', amesema Tony.
Kwa upande wake nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema walijipaga kupata ushindi huo na kama timu hawatabweteka watajipanga kuweza kulinda ushindi wao ugenini.
''Ushindi ni mnono umetupa ulinzi mzuri wa nafasi yetu kwenye mchezo ujao, tuna furaha sana kurejea kwenye michuano hii ya klabu bingwa na kuanza na ushindi wa aina hii'', Mohamed Hussein.