Friday , 19th Aug , 2016

Wakati Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi kesho Agosti 20 mwaka huu, mashabiki wa klabu ya Ndanda ya mkoani Mtwara wamekuwa na matumaini makubwa juu ya timu yao ambayo inakwenda kupambana na Simba katika uwanja wa Taifa DSM

Mshambuliaji wa Simba SC, Ibrahim Hajib (kushoto) na beki wa Ndanda FC, Paul Ngalema katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita

Wakizungumza na Kipenga ya East Africa Radio, baadhi yao wamesema timu hiyo imekamilika na kwamba safari hii wanakwenda kufuta uteja kwa Simba ambayo imekuwa ikiisumbua zaidi Ndanda katika michezo yote waliyokutana katika ligi na ya kirafiki.

Aidha, mmoja wa wanachama wa klabu hiyo na msemaji wa kundi la ushangiliaji la Ndanda Family Wazalendo, Khamis Chichi ameelezea chimbuko la timu hiyo kupewa jina la utani la Wanakuchele.

Kwa upande wake, kiungo anayekipiga kwa mkopo katika klabu hiyo akitokea Azam FC, Bryson Raphael amesema wamejipanga vyema kuelekea mchezo huo na ligi kwa ujumla huku kocha Amimu Mawazo akiwaondoa hofu mashabiki.

Mashabiki wa Ndanda FC
Khamis Chichi, mwanachama wa Ndanda FC
Kiungo Bryson Raphael na Kocha Amimu Mawazo