
Meneja wa sasa wa klabu ya Sunderland Sam Allardyce anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Meneja mpya wa Timu ya Taifa ya England muda wowote kuanzia sasa.
Bodi ya Chama cha Soka nchini, Uingereza inatakaa kumpitisha kama Meneja wao mpya kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliemaliza Mkataba wake hivi karibuni, baada ya kwisha fainali za Euro 2016, na England kutolewa kwenye raundi ya mtoano ya timu 16 na ‘vibonde’ Iceland.
Kwenye mchakato wa uteuzi wa wadhifa huo, Allardyce, maarufu kama "Big Sam", alichuana vikali na Meneja wa Hull City Steve Bruce, aliyewahi kuichezea Manchester United.