Monday , 26th Feb , 2018

Kuelekea mchezo wa raundi ya 19, ligi kuu soka Tanzania Bara leo jioni kati ya Simba dhidi ya Mbao FC, kikosi cha Simba kilichotolewa kimegundulika kuwa na jina la beki Juuko Murshid mwenye kadi nyekundu.

Juuko raia wa Uganda ambaye msimu huu amekuwa nguzo kubwa kwa klabu yake kwa kuisaidia kutoruhusu mabao mengi, alioneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa raundi ya 17, kati ya Simba na Mwadui FC baada ya kucheza rafu.

Kikois kilichotolewa leo jina la Juuko limejumuishwa kama sehemu ya wachezaji wa eneo la ulinzi kwa mujibu wa picha ya kikoki iliyowekwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya klabu hiyo.

Pamoja na baadhi ya mashabiki kuhoji uhalali wa Juuko kuwepo kwenye kikosi cha leo lakini hakuna taarifa ya ufafanuzi ambayo imetolewa lakini pia hata bodi ya ligi haijatoa tamko lolote hivyo sio rahisi kuamini kama Juuko amesamehewa adhabu yake au benchi la ufundi limejisahau.

Simba inaikaribisha Mbao FC ya Mwanza leo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam ikiwa ni mchezo wake wa kiporo baada ya kushinda kucheza kutokana na timu hiyo kushiriki michuano ya kimataifa.