Tuesday , 23rd Jan , 2018

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF litafanya ukaguzi wa mfumo wa leseni kwa vilabu (Club Licencing) kwenye upande wa miundo mbinu.

CAF watafanya ukaguzi huo wa kutembelea na kutazama miundo mbinu ili kuhakikisha mfumo huo unatekelezeka ipasavyo kwa kuanzia na mtazamo wa vigezo vya miundo mbinu.

Kwa mwaka huu 2018 CAF  imeandaa wakaguzi kwaajili ya kutembelea klabu zote zitakazoshiriki hatua ya makundi kwenye mashindano ya vilabu ya CAF hivyo kwa Tanzania vilabu vitakavyogusa ni Simba na Yanga ambao ndio wawakilishi wa nchi kwenye mashindano ya CFA.

Wakaguzi hao  wamejielekeza kwenye ukaguzi wa kiwango na ubora wa viwanja vya kucheza mechi na viwanja vilivyochagua vilabu hivyo kwaajili ya mazoezi ya timu pinzani zitakazokuja kucheza.

Viwanja ambavyo havitakidhi mahitaji hayo ya juu havitaidhinishwa kutumika kwa mashindano na hautatumika kwa mchezo wowote wa hatua hiyo ya makundi kwa mashindano ya klabu kwa mwaka huu 2018.