
Msemaji wa Simba Haji Manara kwenye mahojiano na East Africa Television amesema wao kama klabu wanashukuru lakini uwanja ni uwanja tu na wao wanacheza uwanja wowote.
''Tunashukuru Mungu hatuna la kusema, sisi tunacheza uwanja wowote, uwanja uwanja tu'', amesema Haji Manara. Pia ameongeza kuwa wachezaji wataingia leo jijini Dar es salaam kutoka Morogoro ambako wameweka kambi kwa siku kadhaa.
Mapema leo mkurugenzi wa Bodi ya Ligi ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) Boniface Wambura ametangaza kupata ruhusa ya serikali kuanza kutumika kwa uwanja wa Taifa uliokuwa kwenye matengenezo na utafunguliwa kesho kwa mechi ya Ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Singida United.
Kwa upande wao Singida United kupitia kwa Mkurugenzi wa timu hiyo Festo Sanga wamepokea kwa furaha taarifa hiyo na kuomba uwanja wa Namfua uzidi kuboreshwa ili ufikie viwango vikubwa kama wa Taifa au zaidi.