Monday , 5th Jun , 2017

Singida United imekuwa ya kwanza kuaga michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kufungwa kwa penati 5-4 dhidi ya AFC Leopard ya Kenya kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa AFC Leopard (Waliovalia jezi ya mistari ya blue na nyeupe), Singida United waliovalia kijani.

Mpaka kipindi cha pili cha mchezo kumalizika timu zote zilikwenda sare ya goli 1-1 na kusababisha kuangukia kwenye matuta ili apatikane mshindi wa kwenda moja kwa moja kwenye nusu fainali ya kwanza.

Waliotumbukiza nyavuni matuta ya AFC Leopard ni Bernard Mangoli, Marselas Ingotsi, Kateregga Allan, Duncan Otieno na Fiamenyo Gilbert, wakati za Singida zilifungwa na Atupele Green, Hamisi Shengo, Nhivi Simbarashe na Muroiwa Elisha.

Kikosi cha Singida United kilikuwa; Lubawa Said, Muroiwa Elisha, Msonjo Roland, Dumba Hassan, Chukwu Salum, Ally Kenny, Mtasa Wisdom, Kutinyu Tafadzwa/ Kagoma Yussuf , Green Atupele, Nhivi Simbarashe/ Nizar Khalfan  na Shengo Hamisi.

AFC Leopards; Gabriel Andika, Dennis Sikhai, Marcus Abwao, Abdallah Salim, Duncan Otieno, Isuza Whyvonne, Mangoli Bernard, Joshua Mawira, Fiamenyo Gilbert, Haron Nyakha/Allan Kateregga na Vincent Oburu.