Wednesday , 27th Jan , 2016

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mashindano ya riadha Afrika Mashariki na Kati yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi April mwaka huu kwa kushirikisha nchi 11.

Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzani RT Ombeni Zavara amesema, mashindano hayo yamepangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi April lakini bado wanaendelea kufanya mawasiliano na katibu mkuu wa Afrika Mashariki ili kujua utaratibu mzima wa mashindano hayo.

Zavara amesema, wao kama nchi wenyeji wa mashindano hayo wamepanga tarehe hiyo lakini bado haijapitishwa rasmi kwani hapo awali ilipangwa mashindano hayo yafanyike April 14 lakini walibadilisha ili kuweza kuwapa washiriki muda mrefu wa kuweza kufanya maandalizi.