
Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa habari wa Shirikisho la Soka TFF, Baraka Kizuguto amesema katika mabadiliko yaliyofanywa na kamati ya kuendesha Ligi, Mchezaji Ibrahim Ajibu anahaki ya kucheza mechi ambapo alicheza dhidi ya Tanzania Prisons na pia atacheza mechi ya Simba dhidi ya Yanga lakini hatacheza mechi zinazofuiata kufuatana na maombi waliofanya viongozi wake.
Kizuguto amesema, kanuni hiyo ni halali na ilianza kutumika kwa mchezaji wa Klabu ya Simba Abdi Banda katika Mechi ya Simba dhidi ya Stand United iliyochezwa Mjini Shinyanga.
Kizuguto amesema, kwa upande wa mabadiliko ya ratiba, Timu ya Yanga mara baada ya kumaliza mechi na BDF Februari 14 alitakiwa Februari 19 acheze dhidi ya Tanzania prisons na baada ya hapo Yanga irejee jijini Dar es salaam kucheza mechi dhidi ya JKT Ruvu lakini Yanga walikutana na viongozi wa TFF na iliomba kucheza baada ya kumaliza mechi dhidi ya Tanzania Prisons waunganishiwe na Mbeya City ili wakirudi Dar es salaam wajiandae na mechi dhidi ya BDF.
Kizuguto amesema, mabadiliko hayo yanafahamika yalifanyika baada ya kubadilisha mechi dhidi ya Mbeya City na wameafiki na kutambua kuwa wanatakiwa kucheza mechi dhidi ya Machi 11 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa kabla ya kucheza na AFC Platinum ya Zimbabwe Machi 14 mwaka huu katika hatua inayofuata ya Kombe la Shirikisho.