Monday , 12th Nov , 2018

Klabu ya soka ya Monaco ya Ufaransa ambayo ilitwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini humo msimu wa 2016-17, haijashinda mchezo hata mmoja msimu huu hivyo kumweka matatani kocha wake Thiery Henry lakini nahodha wa PSG Thiago Silva ameibuka na kumtetea.

Thiery Henry

Baada ya mechi ya jana ambayo iliisha kwa Manaco kufungwa mabao 4-0 na PSG ikiwa nyumbani, Thiago Silva alisema Thierry Henry hana hatia kwa matokeo ya Monaco tangu aichukue kwani anahitaji muda zaidi ili kuiweka simu vizuri.

"Hali ya Monaco ni ngumu. Watu huzungumza mengi juu ya kocha mkuu lakini nadhani kwenye hili kocha ana nafasi ndogo zaidi ya kulaumiwa maana kwa miaka miwili tangu washinde kombe hili wachezaji wameondoka na hawakuwa na mbadala wa wenye uwezo mkubwa'', alisema Thiago.

Thiago Silva

Henry ambaye alichukua mikoba ya kocha Leonardo Jardim aliyefukuzwa mwezi Oktoba ameambulia sare moja tu katika michezo yake minne ya ligi kuu aliyosimama kama kocha mkuu.

Monaco itakabiliana na Caen kwenye Ligue 1 Novemba 24, kabla ya kuivaa Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo katika mechi hizo itakuwa inatafuta ushindi wa kwanza ndani ya miezi mitatu.