Kocha huyo ambaye ni raia wa Hispania, jana aliweka historia hiyo baada ya timu yake ya Man City kufanikiwa kuifunga Arsenal mabao 3-0 kwenye fainali ya kombe la ligi.
Pep ambaye alianza kufundisha soka mwaka 2008 akiwa na Barcelona hadi sasa amekuwa miongoni mwa makocha wenye mafanikio makubwa duniani huku akiwa na sifa ya kufundisha soka la kuvutia.

Makombe ambayo Guardiola ametwaa hadi sasa ni La Liga mara tatu, Copa del Rey mara mbili, Bundesliga mara tatu, DFB Pokal mara mbili na UEFA mara mbili. Mengine ni UEFA Super Cup mara mbili, Klabu bingwa ya dunia mara tatu na sasa kombe la ligi.





