Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ubeligji waifikia rekodi ya Ujerumani

Saturday , 23rd Jun , 2018

Timu ya taifa ya Ubeligji imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Tunisia kwenye mchezo wa Kundi G, Fainali za Kombe la Dunia uliomalizika jioni hii na kujihakikishia kucheza hatua ya 16 bora.

Eden Hazard (mwenye jezi ya njano) akikabiliana na mchezaji wa Tunisia.

Ubeligji ambao wamefikisha alama 6 baada ya kushinda mechi zao mbili dhidi ya Panama na Tunisia, pia wameifikia rekodi iliyowekwa na Ujerumani mwaka 2014 ya wachezaji wawili kufunga mabao 2 kila mmoja kwenye mechi moja.

Wachezaji Toni Kroos na Andre Schurrle walifunga mabao mawili kila mmoja kwenye ushindi wa mabao 7-1 dhidi ya Brazil huku Eden Hazard na Romelo Lukaku wakifunga mabao mawili kila mmoja leo hivyo kuifikia hatua hiyo.
 
Mbali na rekodi hiyo mshamabuliaji wa Manchester United Romelo Lukaku ameungana na nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo kwenye orodha ya wafungaji wenye mabao mengi hadi sasa baada ya kufikisha mabao 4.

Eden Hazard na Romelo Lukaku (wenye jezi za njano) wakishangilia moja ya magoli yao.

Msimamo wa Kundi G sasa Ubeligji ndio vinara na wameshafuzu hatua ya 16 bora wakifuatiwa na England yenye alama 3 kwenye mchezo mmoja. Timu za Panama na Tunisia zinashika mkia zikiwa hazina alama hata moja.