Friday , 22nd Jan , 2016

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Amisi Tmbwe amesema umoja na ushirikiano walionao kwenye timu yao ndiyo unaowafanya wafunge na kushinda kwa kila mechi za ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu huu.

Mshambuliaji wa klabu ya Yanga Amisi Tambwe akishangilia moja ya bao alilofunga wakati klabu yake ikiiadhibu Stand United ya Shinyanga.

Tambwe ambaye kwa sasa ni kinara kwa ufungaji akiwa na mabao 13 aliifungia Yanga Hat-Trick kwenye mchezo wa jana wa ligi kuu ya Soka Tanzania bara na kukamilisha ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya majimaji ya Ruvuma.

Nyota huyo wa kimataifa wa Burundi amesema wao kama wachezaji hawana ubinafsi hali inayopelekea kupeana nafasi kama ilivyokuwa jana kwa Donald Ngoma ambaye akiwa kwenye nafasi ya kufunga alimpa pasi Tambwe na kufunga bao la pili.

Mabao ya Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Amis Tambwe yameifanya Yanga irejee kileleni mwa ligi hiyo ikiwa imemaliza mzunguko wa kwanza wa mechi 15 kwa kufikisha pointi 39 sawa na Azam lakini wao wakiwa juu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Matokeo ya mechi nyingine:
Alhamisi Januari 21
Mwadui FC 2 Kagera Sugar 1
African Sports 0 Mtibwa Sugar 0