Monday , 26th Nov , 2018

Kocha wa klabu ya Arsenal, Unai Emery amefichua siri juu ya mafanikio yake katika lugha ya Kiingereza, kuwa ni kutokana na kuangalia mfululizo wa filamu zinazotumia lugha hiyo mara nyingi.

Kocha wa Arsenal, Unai Emery

Emery hakuwahi kucheza au kufundisha nchini Uingereza kabla ya kuteuliwa na Arsenal kuwa mrithi wa Arsene Wenger wakati wa majira ya joto, lakini amekuwa akizungumza Kiingereza kila mkutano wa waandishi wa habari tangu alipojiunga.

Amesema kuwa kitu pekee kinachomsaidia kuboresha ujuzi wa lugha yake ni mfululizo wa filamu inayohusu familia ya kihalifu katika karne ya 20 ya Birmingham ambayo imekuwa ikirushwa na BBC.

"Sasa ninaangalia mfululizo wa filamu ya Kiingereza ya 'Blinders ya Peaky' ili kuboresha Kiingereza changu." ni nzuri lakini ni vigumu kuelewa kutoka Birmingham kwasababu ina fujo sana lakini ni vizuri," amesema Emery.

Emery alipoteza mechi zake mbili za kwanza akiwa na Arsenal lakini Gunners haijapoteza katika michezo 17 katika mashindano yote tangu hapo.

Baaday ya Arsenal kushinda kwa mabao 2-1 dhidi ya AFC Bournemouth katika uwanja wa Vitality imepunguza pengo kuelekea nafasi nne za juu hadi alama moja , baada ya Chelsea kufungwa na Tottenham Jumamosi. Gunners itacheza na Spurs wikiendi ijayo, ikiwa ni 'derby' ya kwanza ya kocha Unai Emery dhidi ya timu hiyo.