Saturday , 13th May , 2017

Kwa mara ya kwanza Sprite kushirikiana na EATV na East Africa Radio leo wamefanya usaili kwa timu 22 zilizowewza kujitokeza kutoka maeneo mbalimbali nchini kuingia katika mashindano ya kumtafuta Mfalme wa mpira wa Kikapu.

Kamishna wa ufundi na Uendeshaji mashindano wa Shirikisho la mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Manasseh Zablon akiwa pamoja na Afisa masoko kutoka EATV na East Africa Radio, Basilisa Biseko

Katika hatua ya kwanza timu zilizosajiliwa ni Tegeta, Leovice, Lord Baden, Tabata, Lycans Mbezi Beach, Tegeta Camp, K-Warriors, DMI, St. Joseph, Mj Junior, Mchenga, Bahari Beach, Street Boys, Street Warriors, Chanika Legends, God with Us, Junior Basket Ball Club, Weusi Basketball Club, Celestial Basketball Team, TMT, Oilers pamoja na KK Squad.

Ikumbukwe mshindi na Bingwa wa mashindano haya ataondoka na zawadi ya shilingi Milioni 10 na Kombe la 'BBALL KINGS 2017', mshindi wa pili atapata shilingi Milioni tatu, huku mchezaji bora akipata shilingi Milioni mbili na kikombe.


Usaili wa pili unatarajiwa kufanyika tarehe 17 mwezi huu katika viwanja vya mawasiliano Ubungo jijini Dar es Salaam.